Machapisho yote ya E Sports Online Media . Dar es Salaam , Tanzania

Publications
https://avalanches.com/tz/dar_es_salaam__kayoko_mwamuzi_mdogo_zaidi_kuchezesha_simba_na_yanga_achana_na_zil600084_14_07_2020

KAYOKO, MWAMUZI MDOGO ZAIDI KUCHEZESHA SIMBA NA YANGA.


-Achana na zile goli nne walizofungwa Yanga juzi Jumapili, siyo mara ya kwanza. Achana na mashabiki waliozimia. Achana na kitendo cha Morrison kususa. Habari kubwa ni mwamuzi wa kati, Ramadhan Kayoko..


-Mwamuzi huyu chipukizi alichezesha pambano hili kwa kiwango cha hali ya juu sana. Sheria 17 za soka zilionekana uwanjani. Hakuwa na presha wala hofu. Inavutia sana.


-Sasa habari kubwa zaidi ni kwamba, Kayoko ameweka rekodi ya kuwa mwamuzi mwenye umri mdogo zaidi kuchezesha pambano la mashindano la watani wa jadi Simba na Yanga. Kayoko kwa Sasa ana umri wa miaka 26 tu.


-Kayoko aliyezaliwa machi 1994, amevunja rekodi ya mwamuzi Elly Sasii aliyoiweka mwaka 2017 ya kuchezesha pambano la watani wa jadi (Simba na Yanga ) katika mchezo wa Ngao ya Jamii akiwa na miaka 27 tu.


-Sasii ambaye kwa sasa ni mwamuzi bora wa Ligi Kuu mara mbili mfululizo, aliteuliwa kuchezesha pambano la August 2017 Katika mchezo huo Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti baada ya suluhu ndani ya dakika 90..


-Kabla ya Sasii, rekodi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Mwamuzi Mstaafu, Othman Kazi ambaye alichezesha pambano la watani kwa mara ya kwanza mwaka 2005 akiwa na umri wa miaka 28 tu. Simba ilishinda 2-0 licha ya kumaliza pungufu baada ya Victor Costa kuonyeshwa kadi nyekundu.


-Hata hivyo ikumbukwe kwamba mwamuzi Jonesia Rukia alichezesha pambano la watani wa jadi (Simba na Yanga) mwaka 2014 wakati huo akiwa na miaka 25. Hata hivyo haikuwa mechi ya mashindano bali tamasha la Mtani Jembe ambapo Simba ilishinda 2-0.


UPEKEE WA KAYOKO


-Pamoja na rekodi hizo za waamuzi wengine mwamuzi Ramadhani, Kayoko anakuwa mwamuzi wa kwanza kuchezesha mechi ya watani wa jadi katika msimu wake wa kwanza ndani ya Ligi Kuu.


-Kayoko ambaye ni miongoni mwa waamuzi Vijana wenye umri mdogo zaidi kwenye orodha ya waamuzi wa Daraja la kwanza nchini, walipandishwa kuchezesha mechi za Ligi Kuu mwanzoni mwa msimu huu hivyo hii ni mara ya kwanza kuchezesha VPL.


-Kama ulikuwa hufahamu ni kwamba, Kayoko msimu uliopita ndio alikuwa mwamuzi Bora kwenye fainali za mabingwa wa mikoa (RCL) zilizofanyika Simiyu pia alikuwa mwamuzi Bora wa Fainali za U20

Show more
0
146
Show more